NA NICKSON TOSI

Wamiliki wa mikahawa na hoteli nchini sasa watalazimika kulipa kati ya shilingi 2,000 hadi 4,000 kwa serikali ili wafanyakazi wao wafanyiwe vipimo vya virusi vya corona.

Waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema hayo alipofika mbele ya kamati ya bunge inayoangazia utendekazi wa serikali dhidi ya virusi vya serikali.

Tangazo hilo lilijiri baada ya serikali kuamua kupunguza ada hiyo kutokana na hatua ya hospitali za kibinafsi kuanza kutoza watu shilingi 8,500 hadi 10,500 kwa kufanyiwa vipimo tu.

“We have now said that for this purpose government hospitals will not offer the services and charge Sh2,000 to Sh4,000 depending on which government facility one goes to,”amesema Kagwe

Serikali kufikia Jumanne wiki jana, iliamrisha mikahawa nchini kufunguliwa japo kwa kuzingatia masharti makali yaliyokuwa yamewekwa na serikali  kama vile kuwapima wateja wao .

View Comments