04 May 2020 1 Min Read
Tanzia! Mwanahabari wa stesheni moja Kibra auwawa akirejea nyumbani
by Yusuf Juma Habari
NA NICKSON TOSI
Mwanahabari wa kituo cha Pamoja Fm Mtaani Kibra Mohamed Hassan Marijan amepatikana kama ameuwawa na genge la wahalifu mtaani Kibra, eneo la Makina asubuhi ya leo.
Marijan alikutana na kifo chake usiku alipokuwa ametoka kufanya kipindi cha Ramadhan .
Alikuwa amehudumu katika stesheni hiyo kuanzia mwaka 2016.