Beautiful-scaled (1)

NA NICKSON TOSI

Taifa la Kenya kando na kubarikiwa rasilmali tofauti na za kuvutia, pia lilibarikiwa wanawakec warembo zaidi na labda wenye ushawishi mkubwa kwa vizazi vichanga vinavyopania kuwa kama wao.

Hapa nimekuandalia baadhi ya wanawake ambao mwaka huu wa 2020, inadaiwa kuwa ndio warembo zaidi nchini. Tazama.

1. Grace Sowairina Msalame

Ni mwanahabari ambaye japo kuwa alizaliwa mwaka1986, urembo wake unasemekana kuwa unawakosesha wanaume wengi usingizi.

2. Sarah Hassan

Chimuko lake ni Mombasa na alizaliwa mwaka 1988. Sarah ni muigizaji na pia alikuwepo kwenye runinga moja ya humu nchini akifanya kipindi fulani.

3. Avril Kenya

Japo umri nao ni mkubwa, Avrili wa miaka 34, amesalia kuwa miongoni mwa wanawake wanaosemekana kuwa na mvutio wa kupindukia.

4. Mayonde

Jina lake halisi ni Diana Mayonde Nduba. Ni mwanamuziki ambaye sauti yake nyororo na ya kutoa nyoka pangoni ilianza kutamba baada ya kuingia katika sanaa ya muziki.

5. Brenda Wairimu

Anafahamika sana katika taaluma yake ya uigizaji wa filamu za humu nchini. Alizaliwa mwaka 1989.

6. Betty Kyalo

Kando na taarifa za hapa na pale zinazomhusisha na wapenzi tofauti nchini, si hoja kuwa Betty ni miongoni mwa wanahabari ambao walibarikiwa urembo kupindukia.

7. Kambua

Alipozaliwa alipewa jina kama Kambua Mathu na hivi maajuzi alitoa ushuhuda wake baada ya kubarikiwa mtoto.

8. Catherine Kamau

Taarifa yangu haingefikia mahali ilipo kwa sasa iwapo singemtaja msichana huyo anayekua kwa kazi sana nchini katika sekta ya kibiashara na uigizaji.

9. Joyce Omondi

Tabasamu pekee yake ni dhihirisho ya jinsi kichuna huyu alivyobarikiwa. Ni mwanahabari pia katika televisheni moja ya humu nchini.

10. Kamene Goro

Amekuwepo katika tasnia ya uwanahabari kwa muda japo maumbile yake huwatoa wengi mate .

Baadhi ya watu wanaosemekana kuwa wamebarikiwa maumbile ama urembo katika taifa la Kenya.

View Comments