kq-pic

NA NICKSON TOSI

Wakenya waliokuwa wanaishi Uingereza na ambao walikuwa wanashinikiza serikali kuwarejesha nchini hatimaye waliabiri ndege ya Kenya Airways na kutia guu katika anga tua ya JKIA Jumatatu usiku.

Wasafiri hao ambao walikuwa wamechagua maeneo ya kuwekwa kwenye karantini, waliwasilisha stakabadhi zao za kuonyesha hali yao ya virsusi vya corona.

Kulingana na taarifa, abiria hao walilazimka kufanyiwa vipimo katika anga tua hiyo ya JKIA kabla ya kuwekwa kwenye karantini.

Ambrose Njeru mmoja wa abiria hao alisema walilazimika kutuma matokeo yao ya upimaji wa virusi vya corona kwa daktari wa JKIA kabla ya kuruhusiwa kuabiri ndege hiyo.

Kila abiria alikuwa analipa shiliongi 53, 544 kwa safari hiyo.

“We were few in the plane. A passenger was required to occupy three seats,” “We wore masks throughout the journey. The process at JKIA was so smooth that we were on our way to quarantine by 11.30pm.”amesema Njeru.

Idadi ya wakenya wanaoingia nchini inatarajiwa kuongezeka kufikia Ijumaa ambapo waliosalia Uingereza watakuwa wakitua.

Aidha, wakenya wanaoishi katika mataifa ya India na Uchina watatia guu lao nchini kufikia Ijumaa pia.

Balozi wa Kenya New Delhi Willy Bett amesema ndege ya kuwabeba wakenya hao itatoka India mida ya saa 5:15 jioni.

Bett ameongeza kuwa ameliarifu shirika la Kenya Airways kuwa baadhi ya wakenya waliokuwa wamewapeleka wapendwa wao kupokea tiba katika taifa hilo wamekosa viti kwa ndege inayostahili kuwabeba.

Yamkini watu 300 ikiwemo watalii wanasemekana kuchukua tiketi ya kuabiri kuja nchini.

View Comments