Rich-Mavoko-and-Diamond-Platnumz

Si siri kuwa msanii wa nyimbo za bongo Rich Mavoko alinyamaza wakati alipotoka katika lebo ya WCB ambayo inasimamiwa na msanii Diamond.

Uvumi ulienea kuwa ilimlazimu auze mali yake yote ili atoke katika lebo hiyo. Hivi majuzi, tulimuona Harmonize akilipa milioni mbili ili awachiliwe na lebo ya WCB.

Kulingana na uvumi ambao unaenea mitandaoni Rich Mavoko hakuwa na bahati kwa maana alishindwa kupata pesa alizoagizwa na kuuza nyumba yake, magari na hata shamba la wazazi.

Si ajabu akaunti yake ya Youtube inasimamiwa na lebo ya WCB.

Baada ya Rich Mavoko kukimya kwa muda, Harmonize amejitokeza na kuzungumzia hali ya msanii huyo, huku akiuliza kama lebo hiyo ina huruma kwa familia ambazo Rich alikuwa anafanya kazi hiyo kwa ajili yao.

"Familia Ngapi Zipo Nyuma Ya @richmavoko ..?? Na zinamtegemea Yeye Kwa Kila Jambo Hasa Hili La Kupata Mkate Wa Kilasiku VP Kuhusu Ndoto Za Familia Hizo Na Zinaishije kwa Wakati Huu…???" Harmonize Aliuliza.

Kwa mara ya kwanza, Konde boy alizungumzia familia ya Diamond na kuuliza kama pesa zimewafunga macho kwa maana hawaoni maovu waliofanyia msanii mwenzao.

 "Ndoto Ngapi Za Wasani Ambao Wanategemea Kuzifikia Hizo Ndoto Kupitia Mavoco ..?? Na Nyuma Ya Hao Wasanii Kuna Familia Nyengine Pia ..?? Jeee Maumivu Malala Miko Ya Wazazi Wake Hasa Mama Mzazi Ambae Ndio Kama Roho Yake …!!! Ushajiuliza Ni Kauli Ngapi Za Uchungu Anazitoa Ambazo Zinaweza Kumpata Kila Anaefurahishwa Na Hili Kwa Makusudi ..???"

Kwa maana Konde boy alilipa kile chake anajua uchungu wa kulipa deni hilo na kutoka katika lebo hiyo. Akizungumzia hali ya Mavoko, Harmonize alikuwa na haya ya kusema,

"Maana Mzazi wa Mwenzio Ni wako Pia Laana Yake Haishindwi Kukupata …!! La Mwisho Kabisa Mgeukie Mwenzio Anaefurahia Na Kuifanya Hii Kuwa Ni Habari Njema Kwake Ya Kumfanya Atembee Kifua Mbele Na Hata Kuandika Mtandaoni Kwa Furaha MAVOCO KAPOTEA muulize Anafaidika Nanini …???" Alizungumza.

Yote tisa kumi, Harmonize alimpa  Rich Mavoko maneno ya busara na ya kumtia nguvu.

"Mungu Anasababu Na Maana Yake Bro @richimavoco Kama Mdogoako Nakuombea Najua Ukimya Wako Unamaana Kubwa Sanaa Ndani Yako Ninachojua Ni Kujiweka Sawa Na Kutuletea Kazi Zingine Tunakupenda Na Tunakuombea Mungu Akufanyie Wepesi…!!! Let’s Go Bro Mdogoako Rafiki Yako Nipo Hapa Muda Wowote…!!!! RAMADAN KAREEM." Aliongea konde boy.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO