EASTLEIGH

Viongozi wanaitaka serikali kuwasaidia watu katika mitaa ya Eastleigh na oldd town Mombasa ambao  ilifungwa jana ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona .

Wamesema hatua hiyo sio haki kwani idadi ya juu ya walioambukizwa virusi hivyo imetokana na vipimo vilivyolenga wakaazi katika sehemu hizo .

Mamia ya maafisa wa polisi wengi katika nguo za raia wamekuwa wakishika doria katika maeneo hayo ili kuhakikisha kwamba hakuna anayeingia au kutoka katika sehemu hizo kwa siku 15 zijazo. Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan amesema kufungwa kwa eneo la Eastleigh kumeathiri vibaya uchumi wa eneo hilo na serikali inafaa kuanzisha mpango wa kuwapa usaidizi wafanyibiashara ambao biashara zao zitalazimika kufungwa kwa kipindi hicho.

" watu wametakiwa kuchagua kati ya kifo na maisha, iwapo wamechagua maisha basi wasaidieni," amesema.

Eastleigh ilikuwa imegeuka kuwa kitovu cha   maambukizi ya virusi vya corona  jijini baada  kusajili visa 70  ilhali Old town ilikuwa na visa 64 .

"Eastleigh  imekuwa ikiangaziwa kwa sababu  vipimo vya watu wengi  vimefaulu katika eneo hilo  sio dhihirisho kwamba mzigo wa corona upo juu kuliko maeneo mengine ya Nairobi," amesema Yusuf .

Waziri wa afya mutahi kagwe hata hivyo amesema hawajazuia kusambazwa kwa chakula kilichopikwa katika maeneo hayo. Vyakula kama hivyo vitauzwa katika maduka, maduka ya jumla na masoko yatakayopewa leseni. Wizara hiyo hata hivyo imeyafunga masoko ya wazi, mikahawa  na  majumba ya kuuza bidhaa yenye maduka mengine ndani kwa siku 15 zijazo.

View Comments