- hamo 1
- hamo 2
- hamo 3
- Diamond 1

Harmonize  na mwenzake katika WCB Diamond awali walionekana kusalia marafiki licha ya  Konde Boy kuondoka lebo ya Diamond lakini sasa yaonekana glavu sasa zimetoka mikononi kwa Hamornize ambaye anamkosoa Diamond kwa jinsi alivyoshughulikia suala la Rich Mavoko .

Ili  kuukatiza mkataba wake na WCB, Mavoko alilazimika kuuza mali yake, nyumba na gari ili kulipa fedha za kuukatatiza mkataba huo. Harmonize ameshangaa mbona Diamond  na familia yake hawana huruma kwa kuivuruga taaluma ya  mavoko ambaye watu wengi walikuwa wanamtegemea kwa ajili ya kipato chake cha muziki .

Konde Boy alilazimika kulipa shilingi milioni 24 ili kuondoka WCB lakini Rich Mavoko hakuwa na pesa  kiasi hicho wakati alipoondoka ndiposa aliamua kuuza mali yake. Inaripotiwa kwamba licha ya kuondoka WCB, bado Diamond ana haki za kumiliki muziki wa Mavoko katika akaunti yake ya Youtube.

Harmonize ameshangaa jinsi Diamond na familia yake wanavyoweza kumuacha Mavoko na jamaa zake wakiteseka kwa sababu ya tamaa yao ya pesa na aliandika;

Ndoto Ngapi Za Wasani Ambao Wanategemea Kuzifikia Hizo Ndoto Kupitia Mavoco ..?? Na Nyuma Ya Hao Wasanii Kuna Familia NyenginePia ..?? Jeee Maumivu Malala Miko Ya Wazazi Wake Hasa Mama Mzazi Ambae Ndio Kama Roho Yake …!!! Ushajiuliza Ni Kauli Ngapi Za Uchungu Anazitoa Ambazo Zinaweza Kumpata Kila Anaefurahishwa Na Hili Kwa Makusudi ..???

Aliendelea kwa kuonya kwamba Chibu anajitia katika hatari ya kulaaniwa  kwani Mavoko alikuwa akitegemewa na watu wengi wakiwemo wazazi wake.

Maana Mzazi wa Mwenzio Ni wako Pia Laana Yake Haishindwi Kukupata …!! La Mwisho Kabisa Mgeukie Mwenzio Anayefurahia Na Kuifanya

View Comments