NA NICKSON TOSI

Wanariadha 12 kati yao wanawake wanne wametiwa mbaroni na maafisa wa polisi wakiwa kwa chumba kimoja wakibugia mvinyo Uasini Gishu, eneo la Eldoret.

Wanariadha hao kumi na wawili niĀ  Julius Lagat, Washington Muigai, Cynthia Cherono, Christine Chemutai, Brian Okwaro, Judy Cheruto, Dismas Kiplimo, Timothy Rotich, Winfrey Atieno, Gideon Kosgei, Alex LagatĀ  na John Mwangi.vSasa watalazimika kuwekwa kwenye karantini kwa siku 14

Kulingana na mkuu wa polisi kaunti hiyo Johnstone Ipara, mmoja wa wakaazi wa Eldoret haswa chumba walichokuwa wamejificha alimtumia video ya makabwela hao mida ya 4 jioni na kuanzisha harakati za kuwashika.

Ipara amesema kuwa baada ya maafisa wake wa usalama kufanya msako kwenye nyumba waliokuwamo, walikuta kuwa kati ya watu hao 12, wanne walikuwa wanawake na kuongeza kuwa wanaendeleza uchunguzi iwapo wanawake hao walikuwa wanariadha pia.

Vinywaji tofauti vilikusanywa kutoka kwa chumba ambacho jamaa hao walikuwa wamejikusanya.

View Comments