- Tanasha 2
- Tanasha 1
- tanasha 3

Tanasha  Donna   amekuwa akiepuka kuiweka mtandaoni picha ya mwanawe  lakini siku ya akina mama Jumapili, aliamua kuuonyesha ulimwengu jinsi mtoto wake huyo alivyokuwa mkubwa.

Tangu alipotengana na msanii wa bongo Diamond, Tanasha amekuwa akiepuka kabisa  kufanya hivyo na hata walipokuwa pamoja na nyota huyo, ni familia yake iliyokuwa ikiwek picha za mtoto wa Diamond katika mitandao ya kijamii.

Tanasha hata hivyo aliamua kuitumia  siku spesheli ya akina mama kuiweka picha ya mtoto  wake huku pia akimshukuru Diamond kwa kumpa kitu kimoja maishani ambacho anakidhamini sana –mtoto wake

Alaindika ;

 “My lil big brown eyes growing so fast. Te amo siempre mi amor.  I am super proud to be your mother, you make me a better person by the day. I pray to God that you grow up to be positive, humble, successful, kind & most importantly God Fearing. I thank your father for blessing me with you as well… My baby NJ  I will always love you & do everything in my power to protect you…  HAPPY MOTHERS DAY TO ALL THE BEAUTIFUL MOTHERS IN THE WORLD. ”

Tangu Tanasha aliporejea Kenya, Diamond hajapata muda na mtoto wake  lakini pia janga la virusi vya corona limezuia watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Wengi wanataraji kwamba wawili hao hawatakuwa na uhusiano wenye machungu kwa minajili ya mtoto wao  Naseeb Junior kwani uhusiano mbaya kati ya Zari Hassan  na Diamond umevuruga  uwezo wao wawili kuwatunza wanao wawili kwa pamoja.

 

View Comments