Hatua ya rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kukosa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao uliwajumuisha viongozi Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda imeibua hisia mseto miongoni mwa wananchi wa mataifa husika hasa wakati huu ambapo mataifa hayo yanakabiliana na janga la corona.

Si mara ya Kwanza kwa Magufuli kukosa kuhudhuria mkutano huo ambao ulikuwa unajadili hatua ambazo zitachukuliwa ili kukabiliana na janga hilo.

Yanajiri hayo huku wengi wakiendelea kushutumu kiongozi huyo kwa kukataa kuweka mikakati mwafaka ya kuzuia virusi hivyo ambavyo vinaendelea kuongezeka kila uchao.

Kwa sasa taifa hilo limetangaza kuwa na visa 509 vya maambukizi ya virusi hivyo huku watu 21 wakiwa wameaga dunia.

Waziri mkuu wa zaamani wa Kenya Raila Odinga akiwa kwa mahojiano na shirika la BBC alisema Magufuli amekuwa akikosa kuwasiliana na wenzake wa EAC swala ambalo huenda likalemaza juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.

“No, I haven’t talked to my friend. I’ve tried to reach him on phone, but I haven’t been successful,”  “[So], I’ve left him a message on SMS.” Alisema Raila

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza pia alikosa kuhudhuria.

Katika mkutano huo ulioandaliwa kwa njia ya video na uliongozwa na rais wa Rwanda Kagame ambaye ndiye mwenyekiti wa EAC, kwa pamoja viongozi hao walikubaliana kufanya kazi pamoja na kubuni mikakati ya kuwekwa kwenye mipaka ili kuzuia maambukizi.

View Comments