- zari 4
- femi 5
- pjimage (1)

Kuna mjadala mkubwa ambao umekuwa akiwaka mitandaoni na katika fikra za wengi kuhusu ni nani anayefaa kumshukuru yupi kati ya Femi One na  Azziad Nasenya  baada ya umaarufu wa wimbo wa Femi   “Utawezana”.

Femi  aliulizwa iwapo alimlipa angalau kitu kidogo Azziad kwa kuufanya wimbo huo kuwa maarufu lakini Femi akajibu kwamba Azziad alikuwa tu miongoni mwa watu walioshiriki shindano la kuudensi wimbo huo. Hilo halijawafurahisha watu wengi mitandaoni wanaohisi kwamba Azziad alikuwa nguzo muhimu sana katika kuufanya maarufu wimbo huo wa Femi One na  Mejja.

Hata hivyo kuna wengi wanaosema kwamba isingekuwa hatua ya Azziad kunengua kiuno chake kwa ustadi akicheza wimbo huo katika tiko tok, wengi hawangeujua wimbo wa utawezana. Wanasema Azziad anafaa kulipwa  mgao wa pesa zitakazotokanana na mafanikio ya wimbo huo.

Kwa kweli Azziad anafaa kupongezwa na Femi kwa kiasi fulani  kwani   densi ya Azziad  ya wimbo huo ilifika hadi katika ulingo wa kimataifa na kuwafanya watu wengi kote duniani kujaribu pia kuiga densi za Azziad.

Sio siri kwamba wimbo wa utawezana ukianza kupigwa, mtu yeyote aliyemtzama Azziad akidensi ataiona Sura ya Azziad  na wala sio ya Femi One.

https://twitter.com/nasirkenya/status/1260095254612639745

Hata hivyo, kuna wanaodai kwamba Azziad ndiye anayefaa kumlipa Femi One kwa kuutumia wimbo wake kujipa umaarufu.

 

View Comments