EYSRzAWX0AAq-9i

Kutokana na hatua ya uongozi wa taifa la Uganda kufunga baadhi ya maeneo kama njia ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona, yamkini asilimia kubwa ya wananchi kutoka maeneo hayo wamefariki kutokana na njaa.

Mwanaharakati Stella Nyanzi na wengine wengi wametiwa mbaroni na asasi kuu za serikali hiyo baada ya kuandaa maandamanon ya kuishinikiza serikali kuwapa wakaazi chakula baada ya kufungwa kwa shughulu nyingi Uganda.

Taarifa hizi zinajiri wakati ambapo taifa hilo limeripoti visa vipya vya maambukizi 21 ambayo yamepatikana baada ya watu 1, 071 kufanyiwa vipimo.

Mashirika ya kutetea haki za kibanadamu yamekuwa yakikashifu zaidi mataifa ya Afrika kwa kuendelea kuwanyanyasa wanaharakati ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki za wenzao.

Taifa la hivi karibuni kushutumiwa ni lile la Zimbabwe ambapo viongozi watatu wa upinzani walipigwa na polisi na hatimaye kutupwa katika barabara kuu ya mji wa Harare.

View Comments