Papa mtakatifu Francis aliongoza ufunguzi wa kanisa la St Peters Basilica katika mji wa Vatican Jumatatu na makanisa mengine ya kikatoliki nchini Italia kuandaa misa ambazo zilihudhuriwa na watu kwa mara ya kwanza baada ya miezi miwili ya kusitishwa kwa shughuli zote nchini humo .

Kanisa hilo la Basilica ambalo Ijumaaa lilifukiziwa dawa ili kuhakikisha kuwa hakuna virusi vyovyote, lilifunguliwa kwa wakristo na wakuu wengine kuifanya sala zao baada ya Francis kuondoka.

Taarifa zimeripoti kuwa waliokuwa wanahudhuria misa hiyo waliambiwa kuzingatia umbali wa mita 1.5, kuvalia barakoa na kunyunyiza vitakasa mikono kwa mikono yao.

Washirika katika makanisa ya Italia watalazimika kuvalia maski huku Makuhani wakiruhusiwa kuendesha misa bila maski na glavu wakati wa kuwapa sakramenti waumini .

Kwa Ruto mimi ng’o! Sankok asema anashirikiana na rais Uhuru Kenyatta

Jumamosi papa Francis aliwaomba Waitaliano kuzingatia vigezo hivyo vipya kutoka kwa serikali ili kusaidia kupunguza usambaaji wa virusi vya corona.

Aidha wakristu watalazimika kupimwa viwango vya joto kabla ya kuingia ndani ya kanisa.