kahaba

Elijah Lorok, sasa amegeuka kuwa omba omba huko Samburu na imekuwa vigumu kwa wengi kuamini kwamba  mwaka wa 2220 alikuwa mtu tajiri sana katika kijiji chao baada ya kufidiwa shilingi milioni 100.

Elijah alikuwa miongoni mwa wakaazi wa Samburu ambao walifidiwa mamilioni ya pesa kwa kujeruhiwa na vilipuzi  vilivyoachwa na wanajeshi wa uingereza walipokuwa wakifanya mazoezi katika eneo hilo. Wengi walipewa kiasi kikubwa cha  pesa  kama fidia  baada ya kushinda kesi dhidi ya serikali ya Uingereza Julai mwaka wa 2002.  Lorok alikuwa miongoni mwa watu 76  kati  228 waliofidiwa na  idara ya ulinzi  ya Uingereza ambapo familia nyingi zilifidiwa takriban  euro elfu kumi. Lorok alijeruhiwa mgu alipokanyaga bomu la ardhini ambalo halikuwa limelipuliwa akiwa na umri wa miaka 12.   Katika familia, yake zaidi ya watu 7 walifidiwa zaidi ya shilingi milioni kila mmoja lakini ni yeye alipewa kiasi kikubwa cha fidia kwa sababu baada ya kujeruhiwa, ililazimu madaktari waukate mguu wake.

Wakati watu walipofidiwa, wakaazi wengi waliopokea malipo hayo walianza kutumia  vibaya pesa zao na  Lorok anafahamika kwa kuyanunua magari manne  kutumia pesa kwa siku moja. Aliingia jijini na binamu yake Lokwer na  katika kampuni ya kuuza magari mapya walinunua  magari mawili ya Mercedes benz, moja la Toyota prado na  na lingine la Toyota cruiser. Inadaiwa siku hiyo walitumia takriban shilingi  milioni 40 kununua magari na bidhaa zingine za kifahari walipokuja Nairobi. Kufikia  Juni mwaka ufuatao wa 2003, Lorok hakuwa amesalia na hata shilingi moja na alikuwa tena amerejelea maisha yake ya hapo awali ya kuombaomba. Wakaazi wengi  wa Samburu waliojua kuhusu kiasi cha pesa alizopewa walishangaa jinsi alivyoweza kutumia pesa hizo chini ya mwaka mmoja na kubaki bila chochote.

Kuna visa vya jinsi baadhi ya waliofidiwa pesa hizo walivyokuwa wakitumia ndege za kukodi kuja Nairobi na hata Mombasa kufanya raha  na hata kuwaleta mamia ya makahaba kwa karamu kubwa kubwa makwao wakati walipokuwa na pesa. Lorok, inadaiwa wakati alipokuwa na pesa, alikuwa akiwalipa watu katika kituo chao cha kibiashara warejee  nyumbani mapema ili waachie kituo kizima yeye na rafiki zake kufanya karamu kubwa  zilizodumu usiku wote. Wakati mmoja alidaiwa kulaghaiwa shilingi milioni 10 na mfanyibiashara mmoja kutoka Laikipia aliyekuwa amemhadaa kwamba wangefungua biashara ya pamoja kwa kuanzisha shamba la ukulima wa mifugo na mazao huko Njoro. Msururu wa wanawake waliokuwa wakimfuata Lorok kila alikoenda uliwashangaza wengi na wakati mwingine katika msafara wake alikuwa na magari takriban 40 kwa wakati mmoja.

Mwaka wa 2019, Lorok alikuwa bado mjini Maralal  akiwafanyia watu kazi za hapa na pale mashambani na hata wakati mwingine alitegemea huruma za watu kununuliwa chakula katika hoteli za vibandani  mjini humo. Alipokuwa na pesa baadhi ya jamaa zake waliofaulu kumpunja mamilioni ya pesa walikuwa werevu na wakanunua vipande vya ardhi katika sehemu za  Kisima, Lodosoit, Baragoi na Wamba –lakini wote hawataki kumuona tangu alipofilisika na walipogundua kwamba hakuwa na lolote la kuwapa.

View Comments