EYnpqw8XQAAItN4-300x225

Gavana wa kaunti  ya Machakos Alfred Mutua amesema ni sharti madereva wa malori ya masafa marefu wanaopita katika kaunti hiyo wawe na stakabadhi za kuonyesha hali yao ya afya kuhusina na virusi vya corona kabla ya kuingia ama kupita katika kaunti hiyo.

Mutua amesema kwa sasa madereva wanaotumia bara bara ya Mombasa watalazimka kutoa stakabadhi hizo kabla ya kuruhusiwa kuingia.

The truck drivers along Nairobi - Mombasa road will now have to produce a document that shows that they have been tested and are free from Coronavirus disease before being allowed to enter Machakos.amesemaMutua

 Amesema stakabadhi hizo zitakuwa za lazima na iwapo kuna yeyote atakayekosa kuwasilisha nakala hizo hataruhusiwa kuingia Machakos.
Ameongeza kuwa madereva hao watakuwa tu na dakika 30 za kujaza mafuta na hata hawataruhusiwa kuegersha magari hayo kwenye kaunti hiyo.
 Na iwapo mmoja wa madereva hao watapatikana na virusi vya corona wakiwa Machakos, mutua amesema hawatakuwa na la kufanya ili kumrudisha katika kaunti aliyotoka.

Amesema kuwa siku zijazo wakaazi wa kaunti hiyo wataanza kupewe barakoa za bure ili kujikinga dhidi ya janga hilo hatari .

"We have contracted our vocational training colleges to produce masks within the coming one or two months. So this process will make sure all Machakos residents from the children to the adults that they receive a free mask",amesema Mutua .

Kufikia sasa kaunti ya Machakos iumesajili visa 3 tu vya maambukizi ya virusi hivyo hatari.