No beef? Ruto alijikaanga mwenyewe asema Atwoli
Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli amesema hana tofauti za kibinafsi na naibu wa rais William Ruto .
Atwoli, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Ruto amesema wawili hao wanatofautiana tu kisera na falsafa za kisiasa .
‘Sina kinyongo na Dp Ruto ,ni mkenya .Na leo anaweza kunialika kwake tule pamoja name pia nifanye hivyo ‘ amesema Atwoli
Kiongozi huyo wa COTU amejitokeza kama miongoni mwa wanaopinga vikali azma ya Ruto kumrithiri rais Uhuru Kenyatta baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.Ameongeza kwamba Ruto ndiye anayefaa kujilaumu kwa hatua ya washirika wake kupokonywa nyadhifa za uongozi katika senate .
Wale ambao tayari wamefurushwa kutoka nyadhifa hizo ni pamoja na seneta wa Elgeyo-Marakwet Kipchumba Murkomen seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki na seneta wa nakuru Susan Kihika . shoka hilo la kuwaondoa washirika wa Ruto kutoka nafasi za uongozi sasa linaelekezwa bungeni .
Kulingana na Atwoli ,Ruto hajaliwa muaminifu kwa rais Kenyatta na ameendeleza kampeini za kuchukua usukani kabla hata muda wa Kenyatta afisini haujatamatika.
Amesema kuondolewa kwa viongozi wanaomuunga mkono Ruto kutoka nafasi zao hakufai kuchukuliwa kama hila dhidi ya viongozi fulani au jamii zao .