Viongozi wa jamaii ya kalenjin wanatathmini hatua wanaozweza kuchukua baada ya hatua namashambulizi ya kisiasa dhidi ya DP William Ruto katika wiki za hivi karibuni .

Licha ya kumpiga kura rais Uhuru Kenyatta  katika chaguzi mbili kuu sasa wameanza kuzingatia uwezakano wa kufanya ushirikiano na vyama vingine endapo  rais Uhuru Kenyatta hatomuunga mkono Ruto kuwania urais mwaka wa 2022 .

Baadhi ya wabunge kutoka Nandi wakiongozw ana mbunge wa  Chesumei  Wilson Kogo,  wametamaushwa na hatua ya kuondolewa kwa washirika wa Ruto katika nyadhifa za uongozi katika senate .

Seneta wa Elgeyo marakwet  Kipchumba Murkomen  alifurushwa kama kiongozi wa wengi katika senate ilhali Susan Kihika alionyeshwa mlango  kiranja wa wengi kabla ya Kindiki Kithure kuvuliwa madaraka kama naibu spika wa senate .Kogo  wamesema hawapingi jitihada za kuleta umoja nchini lakini wanapinga njama za kumzuia Ruto kuchukua usukani wakati rais Uhuru Kenyatta atakapostaafu mwaka wa 2022.

Kogo  na  mwenyekiti  wa kamati ya amani ya Kisumu- Nandi  d Kisumu-Nandi Charles Tanui  wamesema masaibu ya Ruto yamesababishwa na watu wenye ushawishi mkubwa katika afisi ya rais  ambao hawamtaki Ruto kumrithiri Uhuru .

View Comments