EZQfg8EX0AI_dpE.jfif

Masharti ni kwa mkenya wa kawaida tu! Viongozi hapana.Ni usemi unaotamalaki sasa katika mitandao ya kijamii baada ya viongozi kutoka mkoa wa magharibi kusafiri kutoka Nairobi hadi kaunti ya Kajiado kukutana na katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli licha ya Nairobi kufungwa na serikali.

Picha zinazotumwa sasa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha viongozi hao akiwemo waziri wa ugatuzi nchini Eugene Wamalwa,spika wa seneti Ken Lusaka ,baadhi ya magavana na wabunge wakiwa wamekongamana nyumbani kwa Atwali licha ya viongozi wakuu serikali kuwataka wananchi kuheshimu masharti yaliyowekwa na serikali.

Hamaki za wakenya zinajiri saa chache tu baada ya wakenya 40 kutoka kaunti ya Kisumu kutiwa mbaroni na polisi kwa kile walisema walikuwa wanakimbia bila ya kutimiza umbali wa mita moja.

“It is time we called out Kenyan political leaders for the fraud they are. They declare a curfew for Covid-19 and demand we obey but they don’t. They restrict movement but they are moving freely. They say no succession politics but are politicking. What more lies can they tell us?” ujumbe wa mmoja wa wakenya katika mtandao wa kijamii wa twitter.

Walitofautiana pakubwa na hatua ya serikali ya kuwataka wananchi waendelea kutimiza umbali wa mita moja unusu hivi,japo wakati ambapo Atwoli alikuwa anawahutubia wanahabari kuhusiana na maafikio yao kama viongozi wa magharibi ,wote pamoja walikuwa wamerundikana