- rose-muhando
- muha
- rose-muhando-fb

Msanii wa nyimbo za ijili Rose Muhando kwa muda amekuwa kimya, lakini hivi karibuni atakuwa anatutumbuiza na nyimbo mpya, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Rose alitangaza habari hizi njema kisha kuomba msamaha kwa mashabiki wake kwa kuwa kimya.

Baadhi ya albamu zilizo wafurahisha mashabiki wake ni kama vile Nibebemkiatu kivue, yesu na kupenda miongoni mwa zingine.

Awali aliimba nyimbo akiwashirikisha wasanii mbalimbali kama vile msanii Ringtone na kasolo,kwa muda Rose Muhando alilazwa humu kenya akiwa mgonjwa lakini haijawahi tambulikana alikuwa anaugua nini wakati huo.

“Nimekuwa Kimya Sana Tangu Nitoe Wimbo Wangu Wa Yesu Karibu Kwangu. Kwanza Ningependa Nitoe Shukrani Zangu Kwenu Nyie Watumishi Wa Mungu Kwa Mapokezi Makubwa Sana. Ila Kikubwa Ningependa Kuwajuza Mwezi June Naachia Album Yangu Mpya. Hii Album Ina Nyimbo Za Kuabudu na Kusifu. Naombeni Mnipokee kwa Hili Linalokuja. Mungu Awabariki." Alisema Rose.

Mwaka jana Rose alikuwa kwenye mstari wa mbele wa habari baada ya video kutambaa sana akiombewa na muhubiri Jame Ng'ang'a.

Akiwa katika mahojiano msanii huyo alisema kuwa hakumbuki chochote na vile alivyofika kwenye madhabau ya muhubiri huyo alifichua pia alikuwa amealikwa na muhubiri huyo kanisani mwake alipoanza kuumwa na tumbo ghafla.

View Comments