AN6k9kpTURBXy81MWJlZDEyYTdmY2VlYmQ1ZGVlOGM5MmRmZDQ4ZTkzZC5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ametabiri kuwa rais Uhuru Kenyatta atazidi kufanya mabadiliko katika serikali yake huku akisema kuwa mawaziri chuma chao ki motoni.

Nyoro alitabiri na kusema kuwa wiki hii itakuwa mbaya zaidi na Uhuru anaweza kuwavuta kazi nusu ya mawaziri wake mwishoni mwa wiki hii.

Mbunge huyo ambaye ni mfuasi wa naibu rais William Ruto alisema kuwa timu yake inaamini mabadiliko ya Uhuru yatamsaidia kukuza kwa uchumi mara mbili.

Nyoro pia aliwaonya wafuasi wa Tanga Tanga anahofia urafiki na atabasamu ambayo Uhuru alimuonyesha naibu wake siku ya Madaraka ilikuwa  mtego wa kubadili mambo serikalini.

"Traps come with smiles.. Expect a bloody week ahead. It starts tomorrow with NA and by end of the week, half the cabinet will be gone. We hope the economy will now grow by 18% - with compliant rubber stamps, no more blame games

To our comrades at arms, we must have cold prudent judgement, courage while challenged and total commitment to mission. They can behave like Kenya ni yao for now, but morning is coming. We are African and Africa is our Business."Alitabiri Nyoro.

Baadhi ya utabiri wake alioufanya Jumatatu usiku umekuwa ukweli baada ya Uhuru kuwafuta kazi wafuasi wawili wa Ruto katika bunge.

Kinara huyo wa chama cha jubilee alimpokonya kiongozi wa wengi wa Whip Benjamin Washiali na kumpa mbunge wa Navakholo Emanuel Wangwe malaka hayo.

Naibu wa kiongozi wa wengi Cecily Mbarire alipatwa na shoka hilo na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge Igembe kaskazini Maoka Maore.

View Comments