- gpGk9kpTURBXy8zNDY0MDcyOTNkOTJiN2E5ZWE1NjVjZDI4ZmI0MTcwZC5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
- 3vQk9kpTURBXy81MmFhYzNiNDhlNGY0YTJjNDk3ZWRiZWI3ZDI2NmU0Mi5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Watu watano wamepoteza maisha yao baada ya kupata ajali katika barabara kuu ya Nyeri kuelekea Nanyuki, polisi wakithibitisha ajali hiyo walisema kuwa lori na gari ndogo ziligongana ana kwa ana katika eneo la Narumoru.

Ajali hiyo ilitokea Jumanne jioni. Kulingana na National Transport and Safety Authority (NTSA) mwaka huu watu wengi wamepoteza maisha yao kupitia ajali za barabara kuliko mwaka jana.

Aprili NTSA iliripoti kuwa waendesha pikipiki 262 wamepoteza maisha yao kupitia ajali za barabara kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

Pia kulingana na data za NTSA watembea kwa miguu 309 wamehusika katika ajali za barabara huku 86 wakipoteza maisha yao.

View Comments