- khali
- Khaligraph-OG-696x418

Huku maandamano yakizidi kushuhudiwa nchini Marekani kwa ajili ya ubaguzi wa rangi uliosababisha kifo cha George Floyd, wasanii humu nchini walizungumzia jambo hilo na hata wengi kukumbana na kisa hicho humu nchini.

Rappa Khaligraph Jones alizungumzia jambo hilo na kusema kuwa alibaguliwa na mhindi alipokuwa anaenda kununua jumba aliloliona kwenye mitandao ya kijamii.

Khaligraph hakuweza kuingia katika jumba hilo lililokuwa eneo la Lang'ata, kwa maana alikuwa mwafrika.

Rappa huyo aliwauliza watu kwenye mitandao wazingatie jambo hilo ambalo linatendeka humu nchini huku akisema kuwa kuna baadhi ya wananchi ambao wanakubali watu wa rangi au kabila lao kupanga nyumba.

Hasa msanii huyo alizungumzia maeneo ya Lang'ata na Westlands. Swali ni je, ubaguzi wa rangi utazidi kutekelezwa hadi lini na ni lini utakwisha swali ambalo wengi wanaulizana na wanazidi kuulizana.

Alieleza jinsi alifanyiwa wakati huo,

"Mwaka jana nilienda maeneo ya Lang'ata kuona nyumba nzuri ambayo niliona mitandaoni, baada ya kufika huko tulikatazwa kuingia katika nyumba hiyo

Sababu ilikuwa hawakuwa wahindi ilhali walikuwa waafrika, tuliambiwa tu wahindi pekee ndio walikubaliwa kupangisha majumba hayo

Nilijua ni mazishi nilirudi Kayole polepole, sikupewa heshima."Alieleza Khaligraph.

Baadhi ya wasanii ambao walizungumzia jambo hilo ni kama,

ogaobinna: Happened to me last week in Parklands🤷‍♂️🥵
donimran254 if that happens in our own continents😰😰😰😰 how do you expect people to treat us in their continents…..most of it is not about racism…its about what we’ve shown them that it should be.
nazizihirji:Yoooo word !!!! and this has been happening for such a looong time ! They say vegetarians only.. and even if  you are vegetarian as long as u black hupati house.
krgthedon:Indians are the poorest people on Earth they should even treat Kenyans with some respect!!! Kazi yao ni cleaning toilet and other manual jobs elsewhere in the world E.Africa ndio wanafurisha balls 🤣.