Waziri wa afya Mutahi Kagwe sasa anasema kuwa serikali itaanza kuchapisha picha za watu wanaotoroka katika vituo vya maeneo ya karantini ama hospitali ili kutoa ilani kwa umma kuwa watu hao watawaambukiza maradhi ya corona.

Akiwafafanua watu hao kama hatari kwa jamii, Kagwe alisema kuwa serikali imebaini kuwa watu hao waliowekwa kwenye karantini baada ya kupatikana na virusi hivyo walikuwa wanatoroka kutoka kwa vituo hivyo.

Amesema kuwa hakuna kitu kinachozuia wizara kutekeleza hatua hiyo ili jamii kwa ujumla iwe na uwezo wa kuwabaini.

“When we get to a point where we know some people are running away there is nothing to stop the Ministry of Health from publishing photographs in the newspapers and saying that these people have ran away from a quarantine facility and if you see them call the police or us because they are a danger to society,” alisema  Kagwe.

Alisimulia kuwa watu 6 waliokuwa wamepatikana na virusi hivyo katika kaunti ya Turkana walikuwa wamehepa kutoka maeneo ya kutengwa Jumatano japo serikali ilikuwa imefaulu kuwapata.

Aliongezea kuwa hata wale waliopeana taarifa za uongo wakati wa kupimwa ili kukwepa kuwekwa chini ya karantini, serikali imeanzisha mchakato wa kuwatafuta.

“There is nothing like missing contacts, they are missing persons because we have proven over and over again we can and we do track people down. But the question is why are you waiting for us to track you down.” Amesema Mutahi

 Amesema ili taifa kuweza kukabiliana na janga hili ni sharti umma, wananchi wake wajukumike ipasavyo.