EaC4mT7WsAAppDt.jfif

Vih0ja vimeshuhudiwa katika bunge la kaunti ya Kirinyaga baada ya wawakilishi wadi 24 kati ya 33 kulazimika kulala katika bunge la kaunti hiyo wakisubiri mjadala wa kumng'atua mamlakani gavana Ann Waiguru.

Siku za hivi karibuni mzozo wa uongozi umekuwa ukishuhudiwa katika kaunti ya Kirinya kwa kile wawakilishi hao wanasema ni kutokana na ongezeko la ufisadi.

Waiguru anashutumiwa na baadhi ya wawakikilishi wadi kwa kupeana zabuni ama tender kwa kampuni ambazo zinahusika na jamaa zake wa karibu.