Mwanamitindo kutoka Uganda Zari Hassana amekana madai kuwa amekuwa akimtumia mamake Diamond zawadi.

Familia hizo zimekuwa zikiimarisha uhusiano wao huku ikidaiwa kuwa huenda wawili hao wakarudiana siku za hivi karibuni.

Mitandao ya kijamii kutoka Tanzania ilinukuu kuwa Zari alimtuma mama Dangote chakula alichokuwa amekinunua kutoka Afrika Kusini.

Aidha taarifa hizo alizikana na kusema ni udaku tu.

"Lies, I forgot its Udaku (gossip) page (sic)," Zari alisema

Naam, kama njia ya kujukumikia majukumu yake kama baba, Diamond alimtumia mwanawe Tiffah zawadi ya kifahari ambao kwa sasa wanaishi Afrika Kusini na mama yao.

Katika video hiyo, Tiffah alionekana mwenye kujawa na furaha na kumtumia babake video ya kudhihirisha furaha yake.