sagana

Watu watatu wanaripotiwa kufariki baada ya lori mbili kuhusika kwenye ajali katika kivukio cha Sagana, barabara kuu ya Makuyu - Makutano kaunti ya Kirinyaga.

Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa polisi kaunti hiyo Aden Alio amesema malori hayo mawili yaligongana ana kwa ana na kusababisha moto mkubwa uliochangia vifo vya watu hao.

Kulingana na Alio, gari lingine aina ya Toyota Probox lilishika moto japo dereva akafanikiwa kuokoa maisha yake.

Miili ya watu waliopoteza maisha yao sasa imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Murang'a huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.