i-sk9kpTURBXy84NDFmZDVjN2U1ZGNmMzI4MDYwOTExMzRlMmJiMWY3Yy5wbmeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Msanii Kevin  Bahati amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kumwandikia msanii wa bongo ujumbe huku akimshauri kuwa Diamod ni baba yake awache ugomvi ulio kati yao.

Kupitia kwenye mitandao Bahati alisema kuwa hakuwa na nia ya kumkasirisha Harmonize kupitia ujumbe huo.

Kulingana na Bahati ambaye aliachwa kufuatwa na Harmonize kwenye mitandaao ya kijamii alisema kuwa alikuwa tu anamshauri ndugu yake aliyeona anafanya mabaya na alikuwa anataka kuwe na amani kati yake na aliyetambua talanta yake ya muziki.                                                  `

“Mimi sijaongea na Diamond kutoka sijui lini. Nilikuwa tu namshauri kama ndugu. The way wewe unaweza pata kitu uone hiki kitu Bahati anapotea unishauri. Nilitaka tu amake peace na atoke na Amani fulani sababu ukitoka na Amani unapata Baraka pia. Sikutarajia atakwazika." Bahati Alisema.

Akiwa kwenye mahojiano alisema kuwa hajatumwa na Diamond wala mtu yeyote wa kutoka kwenye lebo ya WCB kama vile ripoti zinasema nchini Tanzania.

“Sijatumwa na mtu yeyote kwanza sijaongea na mtu yeyote wa WCB sijui siku ngapi zimepita. Na sijui nani anaweza nilipa mimi anitume. Nina pesa zangu

Mara ya mwisho nikizungumza na Harmonize alikuwa Nairobi miezi kadhaa imepita alikuwa anahitaji usaidizi na ni mimi tu ambaye ningemsaidia.

Ilikuwa saa tisa usiku akanipigia nikatoka nikaenda hadi studio nikachukua nikaenda hadi Hotelini alikokuwa." Alizungumza Bahati.

Kupitia ujumbe aliouandika alisema kuwa Harmonize anapaswa kunyenyekea na kuomba msamaha.