Maafisa wawili wa IT waliowapiga picha ais Uhuru na Raila CBD washtakiwa
Maafisa wawili wa IT wanaofanya kazi katika hoteli ya Stanley sarova wanaitafuta taarifa ya rais Uhuru Kenyatta katika kesi ambayo wameshtakiwa kwa kuzichukua picha za CCTV zilizowaonyesha viongozi hao wawili wakifika katika barabara ya Kenyatta Juni tarehe 2
Wakili wao Danstan Omari siku jumatano amesema pia watamtaka kiongozi wa ODM Raila Odinga kutoa taarifa . Raila na Uhuru walinaswa katika picha hiyo ya Video wakizuru miradi mbali mbali inayoetekelezwa CBD .
Omari amesema wateja wake watazitumia taarifa hizo kama utetezi kwani wamepoteza kazi zao kwa ajili ya kesi hiyo .
Patrick Rading na Janet Magoma walifikishwa kortini jumatano na kushtakiwa kwa kukiuka sharia za kutumia vibaya komputa na uhalifu wa mtandaoni .
Omari amemuambia hakimu Bernad Ochoi kwamba wateja wake hawakukiuka sharia yoyote kwani walikuwa tu wanaonyesha ‘uzalendo’
Inadaiwa wawili hao mwendo wa saa mbili na dakika 20 juni tarehe 2 waliichukua picha hiyo ya video iliyowaonyesha rais Kenyatta na msafara wae katika barabara ya Kenyatta .
Serikali haikupinga kuachiliwa kwao kwa dhamana na kuutaka upande wa utetezi kutoa ushahidi wa kuonyesha kwamba wateja wao wamepoteza kazi zao .
Waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu kumi pesa taslimu