dow

Mwanamme mmoja mmarekani anakabiliwa na kfungo cha miaka 16 jela  bada ya kukiri shtaka la kuwadhulumu kimapenzi  wasichana wanne  katika kituo kimoja cha kuwalinda watoto katika kaunti ya Bomet

Gregory Dow, 61,  alikubali kwamba  alitejeleza maovu hayo kati ya mwaka wa 2013 na 2017 katika kituo hicho ambacho yeye na mkewe walikuwa wakikiendesha .

Chini ya makubaliano na upande wa mashtaka ,Dow atahukumiwa  miaka 15 na miezi minane jela .Atahukuiwa rasmi septemba tarehe 29.

Dow anadaiwa kuwadhulumu wasichana hao  wakati wawili kati yao walipokuwa nanumri wa miaka 11 ,mmoja miaka 12 na mwingine alikuwa na umri wa miaka 13

Dow  alijifanya kuwa mhudumu wa kimishenari wa kikristu  a kuanzisha kituo cha kuwahudumia mayatima  na badala yakuwatunza kama baba alianza kuwadhulumu kimapenzi .

Alitumia nguvu ili kutekeleza dhulma hizo  kwa mujibu wa waendesha mashtaka katika kesi hiyo .

Kituo hicho cha Dow cha utunzi wa watoto kilichoanzishwa mwaka wa 2008 huko Boityo kilifungwa mwaka wa 2017

Maamlaka za Kenya zilijaribu kumkamata Dow mwaka wa 2017 lakini alifaulu kutoroka na kurejea marekani .

Maafisa wa FBI na polisi wa eneo alikokuwa walifaulu kumanasa na kumkamata julai mwaka wa 2019

View Comments