Easf4QnXYAI5hc2.jfif

Jaribio la kutia mbaroni gavana wa Nairobi Mike Sonko katika eneo la Voi litasalia kama kumbukumbu kwa wengi kufuatia namna afisa wa polisi alivyokabiliana naye mbele ya umma.

Kama njia ya kuonyesha upenda,Sonko ameamua kumlipia afisa huyo ambaye hii leo amekipata cha mtema kuni baada ya mwanamke mmoja kumshika mzima mzima mbele ya umma akisema afisa huyo aliyestaafu amekataa kutoa laki 300 za kukithi nmahitaji ya wanawe.

Sonko hata hivyo ,amesema atatoa kima hicho cha pesa ili zisaidie kukimu maisha ya afisa huyo aliyejulikana kama Mureithi.

Mureithi ni miongoni mwa maafisa wa polisi waliokabiliana na Sonko katika eneo la Voi alipokuwa anajaribu kukimbia kutiwa mbaroni na maafisa kutoka DCI.

Akitumia muda wake kupitia ukurasa wa Facebook,Sonko amesema amemsamehe Mureithi na atashughulikia maslahi ya wanawae.

“The Voi Base Commander who handcuffed me becomes a dead beat dad. I do not support domestic violence. I condemn the use of violence in any relationship but pole sana my friend Mr. Mureithi the recently retired Voi Base commander who forcefully handcuffed me with two pairs of handcuffs just to board a police chopper during my arrest at Voi,” aliandika Sonko..

Amemtaka afisa huyo aliyestaafu kwa sasa kukubali iwapo watoto ni wake

 “My humble advice to you, if the baby the woman is alleging is really yours kindly accept the responsibility its just normal part of life and since you are now retired, I’m willing to pay for you the 300,000/= upkeep the woman has been awarded by the children’s court.”