unsc

Kenya  italazimika kungoja kwa muda ili kufahamu leo endapo itakuwa mwakilishi wa Afrika katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Hii ni baada ya kenya kukosa kupata wingi wa kura kukishinda kiti hicho licha ya kupata kura 113 dhidi ya  kura 78 za Djibouti ambayo pia inataka kiti hicho.

Ili kukishinda kiti hicho, Kenya inahitaji kura  zisizopungua 128. Nairobi inalenga kukitwaa kiti hicho ili kuiziba nafasi ya Afrika kusini  katika kipindi cha mwaka wa 2021-22

Endapo Kenya itashinda kura ya Alhamisi  itakuwa mara ya tatu kwa taifa kuhudumu katika taasisi muhimu katika umoja wa mataifa.

India  ilishinda bila pingamizi kuwa mwakilishi wa Asia Pacific  ilhali Uturuki ilishinda urais wa bunge la  mataifa wanachama. Baraza la usalama la umoja wa mataifa lina jukumu muhimu la kudumisha amani na usalama kote duniani.

View Comments