COVID 19:Maafisa watatu wa polisi Kamukunji wapatikana na coronavirus
Polisi katika kituo cha polisi cha Kamukunji watafanyiwa vipimo vya covid 19 baada ya wenzak watatu kupatikana na ugonjwa huo .
Kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kiliripotiwa baada ya polisi mmoja kupatikana na ugonjwa huo baada ya kupimwa katika hospitali ya Ag Khan siku ya ijumaa . Afisa huyo amejitenga nyumbani kwake Ruiru akifanyia matibabu na chini ya uangalizi wa madaktari .
Afisa mwingine wa cheo cha Constable kutoka kituo hicho anayehudumu katika kundi la kushughulikia dharura za matibabu katika chuo cha mafunzo ya DCI South C pia alipatikana na ugonjwa huo na kupoelekwa katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta .
Familia yake imetengwa katika nyumba yao katika nyumba za polisi mtaani kamukunji .
Afisa wa tatu ni mkaazi wa mtaa wa Fuata Nyayo aliyepatikana na virusi hivyo baada ya kupimwa katika hospitali ya Mbagathi siku ya ijumaa .
Siku ya ijumaa Kenya ilisajili visa 117 vya ugonjwa huo na kufikisha jumla ya 4,374.
Wizara ya afya imezidi kuwatahadharisha wakenya dhidi ya kupuuza maagizo inayotoa ili kupambana na usambaaji wa covid 19 baada ya watu wengi kuanza kurejelea shughuli zao za kawaida bila kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa hapo awali
Wakati huo huo shughuli za mahakama katika kaunti ya Mombasa zimesitishwa baada ya maafisa 11 wa idara ya mahakama kupatikana na ugonjwa huo .