Serikali ya kaunti ya Machakos imefunga kwa siku 14 masoko manane  katika maeneo ya  Kangundo, Mwala na mjini  Machakos baada ya visa vya maambukizi ya Corona kuripotiwa katika maeneo hayo.

Waziri wa afya kaunti hiyo  Titus Kavila amesema hatua hiyo itawapa fursa kuyasafisha masoko hayo ili kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa huo.

Hata hivyo baadhi ya wachuuzi wamepinga hatua hiyo wakisema hawajapimwa wala kupewa chakula cha msaada.

Zaidi ya wahudumu wa afya elfu 50 walio kwenye mstari wa mbele wa kukabiliana na ugonjwa wa Corona watapokea mafunzo ya kumhudumia mgonjwa wa Covid 19, matumizi ya mavazi ya kujikinga dhidi ya maambukizi pamoja na mafunzo ya kisaikolojia.

Mafunzo hayo yatahakikisha kuwa wahudumu wa afya kote duniani wana uwezo wa kujukumika wakati huu wa janga la Corona.

Ukosefu wa wataalam wa kuzungumza wa kutosha na walimu spesheli wa kuwafunza watoto wanaougua ugonjwa wa Tawahudi au Autisim unahujumu juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo kama nchi.

Daktari Anthony Akoto anasema baadhi ya watoto hawa hulazimika kusafiri kuenda katika miji mikubwa kutafuta huduma hizo , ilhali mambo yangekuwa tofauti endapo tungekuwa na wataalm zaidi nchini.

View Comments