Watu wengi  ambao hawajabahatika kupata mtu wa kupenda au wamejiingiza aktika mahusiano mengi ambayo hutumbukia na break ups  hawajui tatizo liko wapi.

Ingawaje hakuna zawadi inayopewa kwa walio katika ndoa au  mahusiano, ni hisia nzuri kuwa na mtu anayekujali kuliko vyote. Hilo halina pingamizi. Ila iwapo umekuwa katika msururu wa mahusiano ya kimapenzi na hujaweza kumpata mmoja wa kudumu naye basi kuna tatizo sio tu kwa upande wako bali pia tatizo laweza kuwa kwake. Kabla hujasalimu amri kuwahi kumpata anayekupenda  basi hebu angali sababu hizo huenda ndizo zinazokunyima mpenzi wa kudumu.

 Husikizi, hushauriwi

Mambo ya mapenzi ni kama mtihani na kila mtu ana mswali yake ila ni vyema kujua wenzako waliofaulu walijibu vipi maswali yao? Au hata  waliskiza vipi maswali yao ndiposa wakapata majibu waliohitaji. Wengi  walio na matatizo ya mahusiano ni watu wasioskiza. Wao domo lipo mbele ya sikio na watasema mengi kuliko kutulia na kuskiza. Ushauri wanaopewa pia unapitia sikio moja na kutokomea katika la pili.  Kuwa mtu wa kuskiza kunaweza kukusaidia kufahamu anachosema, anachopenda na hata anachotaka mwenzio katika uhusiano au ndoa.

Hubadiliki ,hutaki kuboreka

Kuna tabia ambazo mtu huiga au huzaliwa nazo ambazo labda sio za kupendeza. Zinaweza kuwa kikwazo katika uhusiano wako na mwenzako lakini kuna watu ambao tabia hizo kamwe hawaziachi! na hapo ndipo mzizi wa matatizo yao yote katika mahusiano umefanya kosa moja zaidi ya mara  mia moja lakini kila wakati kamwe huna fikra ya kujibadilisha ili uache kufanya kosa hilo na ndiposa unaachwa na kila unayempata. Wengine hawana  muda wa kujaribu kubadilisha ili watu bora, jipe ujuzi mpya au zaidi, taka kufahamu zaidi kuhusu mambo.

Hujifahamu, Hujui wataka nini

Wakati mwingine kufeli katika uhusiano au ndoa sio tu kuhusu udhaifu wako kwa kitabia au maumbile bali ni tatizo dogo la mtu kukosa kujijua. Iwapo hujijui basi itakuwa vigumu sana kujua unataka nini au mtu wa aina gani katika uhusiano au ndoa. Kwa hivyo iwapo hujui wataka nini, kila kilicho na fursa  kitajipata katika maisha yako.

Kamwe husalimu amri

Wewe ni mjua yote  na kamwe  hurudi chini katika   mapingano kuhusu lolote.  Hata pakitokea mfinyo wa njia, mwenzako ndiye anayefaa kukupisha wala wewe una haki zote ya kufanya unalotaka.  Katika mahusiano kuna nyakati ambazo unafaa kumpokeza mwenzako ushindi. Atajiihisi kuwa na mchango katika uhusiano huo ila endapo katika kila jambo basi tamko lako ni sheria, huo sio uhusiano, ni udikteta na kamwe mwenzaako hatovumilia wakati utakapozidi kumkandamiza kimaoni na kwa hatua zako.

 Kiburi

Hili halihitaji hata ufafanuzi kwani sote twajua hatma ya kiburi ni ipi. Kuanzia mwenzako yule shuleni aliyekuwa na jeuri zake na sasa maisha yamemponda vibaya. Adhabu ya kiburi katika uhusiano pia ni iyo hiyo ya machozi. Ukiwa na wengi  peupe utaeleza jinsi uko sawa na huhitaji mwanamme au mwanamke katika  maisha yako lakini usiku gizani ukiwa peke yako, upweke kamwe haukuachi na pale utagundua kwamba una kiburi cha kugundua kwamba unafaa kujituliza ili akupende anayekufaa.

View Comments