Muigai

Tume ya uwiano na utangamano  NCIC  imemtaka msanii wa nyimbo za Muigai Njoroge kufika mbele yake kuhusu wimbo wake unaozua utata kwa jina    Ino migunda  unaozungumza kuhusu watu kufurushwa kutoka kwa makaazi yao.

Kupitia barua iliyoandikwa na  kaimu katibu wa tume hiyo Millicent Okatch, Muigai ametakiwa kufika mbele ya tume hiyo Juni tarehe 26  saa nne asubuhi. Endapo atakosa kufika mbele ya tume hiyo kama ilivyoagizwa, Muigai atajitia katika hatari ya kushtakiwa kwa ukiukaji wa agizo hilo. Amesema hana nia ya kupuuza agizo hilo .

 Katika wimbo huo  Ino Migunda –  neno linalomaanisha ‘mashamba hayo’   Muigai ameweza kuzua mjadala kuhusu uhalali na njia inayotumiwa kuwafurusha watu kutoka  mashamba yanayodaiwa kumilikiwa  na serikali. Wimbo kufikia sasa umechezwa mara 650,000  na watu katika Youtube.

“Shamba hili siku moja litagawanywa kwa njia  iliyo sawa kwa sababu haliwezi kukabdhiwa binadamu. Boma moja Kisumu litakuwa mashakani na ukemi utasikika kutoka Nyahururu hadi Kabarak’ amesema msanii huyo katika wimbo huo wake.

Kulingana na NCIC,  maneno hayo ni ya uchochezi  na yanatishia  utangamano wa kitaifa  na uthabithi wa nchi

Ni mara ya pili kwa mwanamuziki huyo  kutikisa ndimi za watu kupitia muziki wake baada ya wimbo wake mwingine kwa jina Tukunia  kukosolewa na kusifiwa na watu  alipolalamikia ukosefu wa maendeleo katika eneo la Mlima Kenya na kumtwika lawama rais Uhuru Kenyatta kwa hali hiyo.

Katika wimbo huo, Njoroge anamksoa rais Kenyatta kutokana na jinsi anavyomtenga naibu wake William Ruto  akifananisha hali hiyo kama kuavya mimba ya miezi saba. Hata hivyo, katika mahojiano na gazeti la The Star, Njoroge amekana kwamba alilipwa na Ruto kuutoa wimbo huo.

View Comments