Jamaa wanne walionaswa kwenye kamera za siri wakimwibia mtu katika mtaa wa kilimani jijini Nairobi hatimaye wametiwa mbaroni, taarifa ambazo zimethibithshwa na DCI.

Katika taarifa, DCI imesema kuwa jamaa hao walimwibia mtu huyo majira ya asubuhi Jumatatu Kilimani.

Makachero kutoka afisi hiyo hata hivyo wamesema washukiwa hao walipatikana eneo la Kawangware, Gatina na Pangani.