Dkt Rashi Aman amesema baada ya sampuli za watu 2,419 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 kuhusiana na virusi vya corona,watu 176 walipatikana na virusi hivyo na hivyo kufikisha wagonjwa 6,366 walioathirika kutokana na corona.

Wakati uo huo watu 26 waliokuwa wamelazwa hospitalini wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 2,039 waliopona.

Aidha wagonjwa wanne wamefariki na kufikisha watu 148 waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Kati ya visa hivyo vipya ,wanaume ni 100,huku wanawake wakiwa 76.

Waathiriwa ni wa kati ya miaka 3 hadi 78.

Visa 99 vimetokea kaunti ya Nairobi huku kaunti ya Mombasa ikisajili visa 20 kati ya vile vilivyosajiliwa hii leo.

View Comments