Vikwazo vya usafiri  huenda vikaondolewa na serikali baada ya uzinduzi wa  mwongozo wa  taratibu za utalii ,afya na usalama .

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i  amesema taifa sasa lipo salama kwa usafiri . Matiang’I amesema serikali itazidi kuimarisha usalama na kusimamia  shughuli zote za uangalizi ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona .

Amesema hali ilivyo sasa itawalazimu wakenya kujifunza kuishi na virusi vya corona  huku juhudi za ulimwengu mzima kutafuta tiba zikiendelea .

Kauli yake hiyo imekaririwa pia na waziri wa Afya Mutahi Kagwe.serikali ilisitisha usafiri wa aina yoyote  wa kimataifa mwezi aprili  ili  kuthibiti maambukizi ya covid 19 .

View Comments