02 July 2020 1 Min Read
Wanafunzi 15 waliorejea nchini kutoka Sudan wapatikana na Covid 19
by Yusuf Juma Habari
Wanafunzi 15 walowasili maajuzi Mombasa kutoka Sudan wamepatikana na virusi vya corona .
Waziri wa afya wa kaunti ya Mombasa Khadija Shikely amesema wanafunzi hao walikuwa katika kundi la wanafunzi 129 waliosafirishwa kutoka sudan wikendi iliyopita . Walitua katika uwanja wa ndege wa JKIA Jumamosi wiki jana baada ya kusafiri kutumia ndge ya KQ
Walifanyiwa ukaguzi wa matibabu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege kabla ya kupelekwa katika shule ya serikali ya Kizingarea ili kuwekwa karantini kwa siku 14.