bhang-

Wasichana wawili wametiwa mbaroni wakijaribu kuingiza misokoto ya bangi 17  katika kituo cha polisi cha Kianyanga kaunti ya Kirinyaga.

Inadaiwa kuwa washukiwa hao walikuwa wanampelekea jamaa aliyekuwa amezuiliwa kwenye kituo hicho misokoto hiyo ya bangi.

Washukiwa hao Fridah Njeri na  Doreen Wambui wa miaka 18 na  22 wanasemekana walikuwa wanataka kumjulia hali  James Muriithi ambaye alikuwa ametiwa mbaroni kwa kujihusisha na uuzaji wa bangi.

Maafisa wa polisi katika kituo hicho aidha wamesema kuwa wasichana hao walipofika katika kituo hicho,walilazimishwa kufungua chupa iliyokuwa imebeba misokoto hiyo.

Kwa upande wao wasichana hao ,wamesema mwenzao Muriithi aliwapigia akiwambia ni mgonjwa kwa sababu hakuwa amevuta bangi.

” He asked us to use the method saying he feels unwell as he has not smoked in over two days,” Wambui