mudavadi

Inatokota njama ya kuwaondoa  kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na wa FoRD Kenya Moses Wetangula kutoka kilele cha siasa za Magharibi .

Gazeti la the Star limegundua kwamba   mkuu wa COtu Francis Atwoli , gavana wa kakamega Wycliffe Oparanya na waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa wanalenga kuwazika katika kaburi la kisiasa wawili hao .

Ambi hiyo ya   Oparanya na Wamalwa imeonekana kupata uungwaji mkono wa rais Uhuru Kenyatta . Oparanya ni mshirika wa karibu wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga  ni naibu kinara wa chama cha ODM

Mudavadi    na  Wetang’ula  awali wametambuliwa kama viongozi wenye ushawishi mkubwa katika eneo la magharibi na njama hiyo mpya huenda inalenga kupunguza makali yao kisiasa na pia italemaza ajuhudi za viongozi wa jamii ya waluhya kuwa na usemi mmoja wakati wa  uchaguzi mkuu wa 2022

Rais Uhuru Kenyatta wiki hii amekutana na baadhi ya viongozi kutoka eneo hilo la kuwaahidi miradi kadhaa ya maendeleo  lakini Mudavadi na Wetangula hawakualikwa katika mkutano huo .

Duru zaarifu kwamba rais Kenyatta aliahidi kuyafuta madeni ya  kampuni ya sukari ya Muamias ili kuisaidia kufufuliwa .

Kufikia mwezi februari  Muamias ambayo kwa sasa ipo chini ya mrasimu ilikuwa ikidaiwa shilingi bilioni 4.8 kando na pesa inazodaiwa kama kodi na faini .

Ahadi hizo zimejiri siku chache baada yaukarabati wa uwanja mdogo wa ndege wa kakamega kuanza ili kuufanya kufikia kiwango cha kimataifa .  Haijabainika iwapo rais Kenyatta ametofautiana kabisa na Mudavadi ,ambaye wakati mmoja mwaka wa 20132 nusura amuachaie  nafasi ya kugombea urais .

View Comments