Leo katika kipindi cha patanisho mwanamume mmoja aiyefahamika kama Stephen Muthui alipiga simu na kusema anaomba apatanishwe na baba yake mzazi hii ni baada ya kukosana alipookoka na baba yake kudai kuwa ana majini.

"Nilipookoka baba yangu aliniambia kuwa nimekuchua majini na kunifukuza nyumbani, mwaka wa 2015 aliita watu ili wanifukuze nyumbani licha ya yangu ya kujenga

Pia alinisingizia kuwa ni mimi kiini cha dada zangu kutoka kwa ndoa zao na kurudi nyumbani nilipomuuliza sababu aliniambia kuwa ni majini zangu zimesababisha hayo

Nilihama kwetu baada ya kufukuzwa, baada ya kuhama baba hakutosheka baba alibomoa nyumba yangu." Alieleza Muthui.

Baba yake Muthui alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi ni mkristo na sababu ya kumfukuza mwanangu ni kwa maana anaushirikina mwini lich ya kusema ameokoka."

Baada ya vituko hivyo vyote Muthui alichuwa hatua ya kuenda kwa wazee wa kijiji, kwa kasisi hata kuenda kwa OCS lakini nguvu zake ziliambulia patupu.

View Comments