No apologies !Anita Nderu asimama kidete na uamuzi wake wa kuwaleta mashoga katika kipindi chake
Mtangazaji Anita Nderu amesimama kidete na uamuzi wake wa kuwaleta mashoga katika kipindi chake cha upishi Instagram. Akizungumza na Massawe Japanni katika kipindi chake cha Ilikuaje kwa njia ya simu ,Nderu amesema ingawaje anaheshimu maoni ya watu na misimamo yao kuhusu ushoga ,katu hataomba radhi kwa uamzi wa kuwaleta rafiki zake hao ambao ni wapenzi wa jinsia moja
https://www.instagram.com/p/CCL3S8Uhom9/
Nderu alizua mhemko mtandaoni baada ya kurushiwa cheche za shutuma na watu wengi kwa kuwaleta wapenzi wa jinsia moja katika kipindi hicho ambapo walionekana wakipika na kufanya densi densi mtandaoni . baadaye watu wengi walianza kumtumia jumbe za kumkashifu kwa upotofu wa maadili wakimtaka aiondoe video hiyo mtandaoni lakini hajatikisika .
Alipoulizwa na Massawe iwapo naye pia ni shoga amesema hilo ni jambo la kibinafsi na atajitokeza endapo itahitajika au wakati ufaao ingawaje kwa sasa amebainisha wazi kwamba anaunga mkono wa jamii ya LGBTQ.
https://www.instagram.com/p/CCIEZkBh7RG/?utm_source=ig_embed
Ameongeza kwamba hatosita kuwaleta tena watu wa jinsia moja katika makala yajayo ya kipindi chake instagram kwani kila mtu anafaa kuheshimu maoni ya wengine .
‘Nakataa kuomba msamaha kwa kuwaruhusu rafiki zangu kuwa jinsi walivyo,nakataa kuomba msamaha kwa kupeperuha episode hiyo kwa sababu ni yangu ,ingawaje naheshimu uamuzi wa wale ambao hawajapendezwa na kipindi hicho’