police

Watu watatu wamekamatwa kwa  utekaji nyara na kitisha fidia ya shilingi elfu 150 ili kumuachilia mateka wao huko Meru .

Patrick Kimathi, Joseph Karithi   na  Daniel Muroki   wote walio na umri wa chini ya miaka 30 walikamatwa baada ya ripoti ya  mtu aluyepotea kuwasilishwa kwa polisi .

Maafisa wa  DCI   wamesema ripoti hiyo ilikuwa imewasilishwa kwa kituo cha polisi cha Kangeta ,Meru juni tarehe 19  mwaka huu .

Makachero kwa ushirikiana na polisi kisha walianza oparesheni  iliyopigwa jeki na habari za ujasusi katika eneo la Kiutune ,Igembe ya kati  . Polisi hao walielekezwa katika msitu wa Njuri Ncheke  katika kijiji cha mpinda ambako washukiwa walionekana wakijaribu kutoroka  lakini wakakamatwa kwa usaidizi wa wananchi .

Watatu hao kisha  waliwaelkeza polisi katika kichaka kilichokuwa karibu ambapo  mateka wao aliokolewa baada ya kuzuiliwa katika eneo hilo kwa siku 14 .

Mwathiriwa alipelekwa hospitalini kwa uangalizi huku washukiwa wakizuiliwa na polisi  na vitu kadhaa kuchukuliwa katika eneo la uhalifu ili kutumiwa kama ushahidi .

 

View Comments