IMG-20200706-WA0001

Kikundi cha wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia mchezaji wa zamani wa AFC Leopards Martin Imbalambala ambaye alipoteza uwezo wa kuona.

Korea kama alivyokuwa anafahamika, alipoteza uwezo wake wa kuona mwaka 2018 siku chache tu baada ya kutangaza kustaafu kutoka kwa ulingo wa soka.

Msaadi huu unajiri baada ya taarifa kuchipuka kutoka kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha Imbalambala na mkewe Jackline wakitaka msamaria mwema kujitokeza ili kusaidia gwiji huyo.

Hiyo jana, Shirika la  Macleans Sloya Foundation lilitembelea familia ya gwiji huyo nyumbani kwake Kisatiru na kuamua kumfanyia bajeti ya nyumbani.

Mkurugenzi wa shirika hilo Igaanza Sloya pia amehaidi kumpeleka Imbalambala katika shule ya walemavu wa macho.