Tarehe saba Julai ni siku ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mama yake staa wa bongo Diamond na baby mama wake Tanasha Donna.

Mwaka huu mambo yalikuwa tofauti na mwaka jana. Mwaka jana msanii Diamond alihakikisha mama Dangote na Tanasha wamesherehekea siku hiyo maalum kwa njia ya kipekee huku akiwawekea sherehe ila mwaka huu mambo hayakuwa vile.

"WORDS CAN’T EXPRESS HOW HAPPY I AM TO CELEBRATE THE REBORN OF THE TWO WOMEN THAT I LOVE THE MOST… MY LOVELY MOM @MAMA_DANGOTE AND LOVELY BABY @TANASHADONNA." Ujumbe wa Diamond wa mwaka jana.

Jana familia ya staa huyo ilimtakia mama yake siku njema ya kuzaliwa hata wanawe akiwa na Zari ilhali hamna yeyote aliyemtakia baraka au siku njema kwa Tanasha licha ya kuwa siku muhimu kwake.

https://www.instagram.com/p/CCVEMlPhmNa/

Sandra aliposti video ya Naseeb Junior mwanawe Diamond na Tanasha huku akijifunza kutembea na kusema kuwa ni zawadi ya kipekee katika siku hiyo.

"KWELI LEO NIMEONYESHWA SURPRISE NA BWANA NASEEB TOM KAKA KASIKIA LEO MKEWE KAZALIWA NA YY KATEMBEA KWELI BWANA NASEEB ANANIPENDA ANATAKA AJE AFURAHI NA MM MKEWE." Aliandika Sandra.

Diamond naye hakuachwa nyuma bali alikuwa na haya ya kuandika kwenye video hiyo.

"LION……🔥🦁🔥."

Tanasha hajakuwa kwenye mahusiano mema na familia ya Diamond na pia Diamond mwenyewe, baada ya kuachana mapema mwaka huu. Swali kuu ni je, nani alimtumia Sandra Video hiyo Tanasha au mfanyakazi?

Hii hapa video ya Naseeb Junior akijaribu kutembea;

https://www.instagram.com/p/CCW4Nauh9tI/

View Comments