Katika awamu ya patanisho hii leo, mama Winfin  alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe aliyeachana naye mwaka wa 2016 baada ya kwenda nje ya ndoa.

"Kabla ya kutengana na mume wangu tulikuwa katika ndoa kwa muda wa miaka mitano. Tulikuwa tumebarikiwa na watoto wawili, lakini mmoja aliaga dunia mwaka wa 2017

Tulitengana mwaka wa 2016 baada ya kumuuliza kwa nini ananihanya, nilikuwa nikifua nguo napata vitu ambavyo alikuwa ametumia na mwanamke mwingine kwenye lodging

Kuna wakati aliacha simu kwa nyumba, kuangalia nikapata mambo ambayo alikuwa anafanya na msichana huyo. Cha kushangaza huyo msichana nilikuwa namfahamu, siku moja nilipomuuliza kwa nini anaenda nje ya ndoa alikusanya virago na kuniacha peke yangu

Mwaka jana tulipatana akaniambia tutarudiana Januari lakini nilipompigia simu hakupokea simu zangu."

Yote tisa kumi ni kuwa mama Winfin alipobeba mimba yake ya tatu Martin alisema kuwa hiyo mimba si ya kwake, ina maana  hajawahi ona mtoto wake.

"Nilipozaa huyo mtoto nilifanyiwa upasuaji. Kwenda kwa mume wangu, mzazi mkwe aliniambia kuwa wanawake ambao wamefanyiwa upasuaji hawapaswi kukaa kwa hiyo boma

Waliniambia niende watasaidia mtoto wangu." Alieleza.

Martin alipopigiwa simu hakupokea. Je, unaweza mshauri mama huyo vipi? Kwa uhondo zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.

View Comments