- kate-actress
- Kate-Actress-7

Muigizaji Catherine Kamau almaarufu Cate Actress  na rafikiye Faith Nyagah wanawapa wanawake wengi ushauri wa kuendelea na maisha yao baada ya kuachwa na wapenzi wao licha yao kuwa na watoto wao.

Cate na mwenzake kwa muda wamekuwa wakiwalea wana wao peke yao au ukipenda wamekuwa 'single mothers.'

"Endapo ujipate kwenye hali hiyo kubali yaliyotokea, itakusaidia kupona kutoka hapo itakuwa rahisi sana kwako kuendelea na maisha yako

Kufikia sasa, kuna wanawake wengi ambao wamewaficha watoto wao kwa maana hawajakubali matokeo, sababu ya wasichana wetu kuchagua kuavya mimba ni kwa ajili wanaogopa unyanyapaa wa jamii

Kile watu wanazungumza hakiwezi kubadilisha hali." Alisema Faith.

Cate alisema kuwa alikuwa anajitambulisha kama mama aliporudi kuchumbiana.

"Ikiwa ulifanya uamuzi mbaya au la tayari mtoto yuko hapa, watu wanaweza fikiria kuwa huyu ni malaya kwa maana alipata mtoi akiwa mdogo

Kuna wakati utapatana na mtu mzuri, kuna wakati nilipata kazi na nilipatana na Boujee guys nuliwaambia jina langu na mimi ni mama walishtuka sana

Wasichana niliokuwa na wao walishindwa kwa nini nilijitambulisha vile, sasa nitawaficha hadi lini? Wanaume wengine huwa wanafikiri wanakuchumbia kukupa tu fadhila

Kuna mtu aliniuliza unanikataa unadhani unaolewa na nani." Cate Alizungumza.

Walisema haya kwenye mitandao ya kijamii yake Cate ya Youtube.

View Comments