Covid 19:Watu 447 wapatikana na corona na kufikisha visa hivyo kuwa 8975 nchini
Kenya leo imesajili visa vingi zaidi vya watu walio na ugonjwa wa corona kwa siku moja baada ya watu 447 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo na kufikisha jumla ya wagonjwa wa corona kuwa 8,975
Idadi hiyo ndio ya juu zaidi tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha ugonjwa huo nchini. Visa hivyo vipya vimetokana na sampuli 3,803 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.
Jumla ya sampuli 200,311 zimepimwa hadi kufikia sasa, amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe. Katika visa hivyo vipya, 280 ni vya wanaume ilhali 157 ni vya wanawake.
Wagonjwa 64 wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha watu 2,657 waliopona ugonjwa huo.
Akizungumza huko Mombasa, waziri Kagwe amewasifu maafisa wa kaunti hiyo kwa mikakati waliochukua kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa wa corona. Kaunti hiyo kwa sasa ina visa 1,663 vya wagonjwa wa corona na Kagwe imesema idadi hiyo itaongezeka.
Ameihimiza serikali kuwapa shinikizo viongozi wa kaunti kuzingatia masuala ya afya katika mipango yao .