Wakenya wagadhabishwa na hotuba ya Edwin Sifuna kwa ajili ya ripoti ya runinga ya NTV kuhusu DJ Evolve na Babu Owino
Baadhi ya wakenya katika mitandao ya kijamii ya twitter wamegadhabishwa na maoni au hotuba ya katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna kuhusu habari za runinga ya NTV inayomhusu mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na DJ Evolve.
Mbunge huyo alimpiga risasi Evolve kwenye shingo mapema mwaka huu.
Kupitia kwenye mitandao hiyo, Sifuna alisema licha ya wanahabari, Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) na mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai (DCI) kuzuiliwa kuzungumzia kesi hiyo walienda kinyume na maagizo ya jaji aliyepeana maagizo hayo.
Alizidi na mazungumzo yake ya kusema kwa ajili ya habari au ripoti yao, jaji huyo anaweza kujiondoa kwa kesi hiyo na kusababisha kukawia kwa uamuzi wa kesi hiyo.
“You shouldn't have to be told not to discuss merits of a case . I watched this piece jana and you basically accused the judge of impropriety for this order "granted in darkness". You geniuses will cause the judge to recuse himself causing further delay to the case." Aliandika Sifuna.
Ni matamshi ambayo hayakumuendea vyema huku baadhi ya wanamitandao wakimwambia kuwa amemuunga Babu Owino mkono kwa sababu ni mwanachama wa chama cha ODM.
Pia wengi walitaka kujua kwa nini anamtetea Babu na ni nini haswa muhimu kuhusu kesi hii.
Hizi hapa baadhi za hisia za wanamtandao;
Matt MW Senior :Pple of Kanduyi want you, to return them that ONE vote, that gave you in 2013.Shame on you.